Vitabu Ninavyotaka Kusoma Katika Mwaka 2018

Reading Time: 4 minutes

                  

  “Mwaka mpya, mambo mapya”
Mimi napenda kusoma vitabu, napenda sana kiasi kwamba hata kwenye bio yangu nimeweka hilo swala. Nadhani kuna ujuzi na maarifa mapya ambayo yanapatikana kwenye vitabu, kuna vitu vingi sana unavyoweza kuvipata kutokana na kusoma vitabu. Kuna msemo unasema kwamba “ukitaka kumficha mwaAfrika hela au dhahabu, iweke kwenye kitabu”, ni wazi kwamba mimi nitaipata hiyo hela au dhahabu kwa maana nasoma. Japo kuwa huu ni msemo wa matani tu, lakini bado nashauri watu wasome vitabu, kupata ujuzi usiokuwa na gharama kubwa sana.
 Kuna sababu nyingi watu hawasomi vitabu, na moja wapo ambayo nimeisikia sana ni gharama, jamani sikuhizi vitabu unaweza ukavidownload hata online, mwishoni nitaweka link ambayo huwa natumia kupata vitabu mtandaoni ambavyo vinapatikana bure. Lakini pia jamani kama kweli una nia sidhani kama utakosa njia ya kupata kitabu cha kusoma, na kama hivyo basi hata Biblia hauna, maana nayo unanunua jamani.

Leo tumeuanza mwezi wa tatu wa mwaka huu mpya. Kwahiyo kwa list ninayoitoa hapa inatakiwa kuwe kuna vichache nilivyovisoma ??, okey vichache nimevisoma.
Mwaka huu nataka nisome sana vitabu ambavyo tayari ninavyo, maana nazidi kukusanya vitabu ambavyo sivisomi, maana hivi nilivyonavyo vingi nilivikusanya mwaka jana??, kwahiyo mwaka huu naomba nivimalize hivi kwanza.

Sasa mwaka huu nataka kusoma vitabu vifuatavyo:

Hiki ni kitabu ambacho nimekisoma tayari mwezi wa kwanza, ni kitabu kinachoongelea ndoa kwa jicho la tofauti sana, ni jinsi gani ndoa inaweza ikabadilisha vile tunaishi maisha yetu, badala ya kuishi tu kama wanandoa kwaajili yetu sisi, ni jinsi gani tunaweza kuishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Na nilivomaliza kusoma hiki kitabu nimewashauri marafiki zangu wengi wa kisome. Hiki kinapatikana kwenye website yao ambayo ni hiyo link hapo, au kwenye Playstore, kama application. Mimi pia nimekisoma kama application.

Hiki kitabu ndo nimekianza na ndo ninachokisoma sasa,lakini kinahusu jinsi gani ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi kama amri ambayo Mwokozi na Bwana wetu alituachia. Napenda sana umishenari na kujua jinsi gani ya kuwahubiria na kuwafanya watu kuwa wanafunzi. Toka nimfuatilie Francis Chan amekuwa akifundisha ni jinsi gani ya kufungua milango ya kanisa na watu kuacha kukaa tu kanisani bali kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi, nimekianza tu, na nimekifurahia. Kinapatikana kwenye website kwenye hiyo link hapo juu lakini pia ninaweza kutumia kwa email kama utaacha comment ya email yako hapa chini.

Hiki kitabu nimekisoma katika group ambalo nipo la wadada, ndo kitabu ambacho tunakisoma sasa. Ni kwaajili ya wanawake, na jinsi gani tunaomba lkini ni vitu gani vinatuzuia kuomba ambavyo adui anavitumia. Ni kitabu kinachobadilisha maisha yangu na sitabaki kama nilivyo baada ya kukimaliza.

Hiki bado sijakianza kukisoma, ila ni kitabu ambacho natamani nikisome na nitakisoma katika mwaka huu. John Piper ni mwandishi ambaye nimemfuatilia tangu siku ambayo niliona movie ya 90 minutes in Heaven, na nimekuwa msomaji mzuri wa blogu yake ya Desiring God, na nikimfuatilia mahubiri yake. Kwahiyo najua hiki kitabu kitakuwa kizuri sana. Unaweza kukipata katika hiyo link pia.

Hiki ni kitabu cha kujitambua unaongea lugha gani au unaelezea upendo kwa namna gani, kutokana na uchunguzi alioufanya mwandishi ni kwamba kuna lugha tano ambazo watu wanaziongea au wanazitumia kuonyesha upendo kwa wengine, kwahiyo nataka kusoma hiki kitabu ili nijitambue zaidi. Katika hizo  lugha tano yangu ni ipi.

Hiki nimesikia watu wengi wanakisifia kuwa ni kitabu ambacho kinaelezea jinsi ya kuweza kusubiri na kujitunza mpaka kumpata mwenzi lakini pia jinsi gani mnaweza kusubiri pamoja mpaka ndoa ndipo mfanye tendo la ndoa, kwa maana waandishi pia walisubiri mpaka ndoa. Naona ni kitabu kizuri maana katika dunia hii ambayo inarahisisha sana tendo la ndoa, hiki ni kitabu kinachoweza kukutia moyo haswa ukizingatia waandishi pia ni watu maarufu lakini wameweza kufanya vile Mungu anatuagiza.

  Hiki kitabu nimevutiwa sana na kichwa chake cha habari, na ndi sababu kuu ya kukinunua. Kinaelezea wanwake mbalimbali kwenye Biblia ambao walikuwa hawako vizuri na Mungu na ni mambo gani tunaweza kujifunza kutoka kwao. Kwahiyo siwezi kusubiri kukisoma, nakujifunza kutoka kwao kwa jicho la mwandishi.

Hiki nimekipenda sana japo sijaanza kukisoma, kwasababu kinaelezea ni jisni gani wanawake waliokuwa waaminifu kwa Mungu waliishi na jinsi gani Mungu aliwatokea kwenye hali zao mbalimbali. 
Ninataka kusoma hiki kitabu kwasababu natamani kujua safari yake mpaka alipompata Kristo, kinaweza kikawa kinafanana na kitabu cha Tortured For Christ- Richard Wurmbrand, ambacho kilibadilisha maisha yangu mwaka jana, na nilisoma jinsi waKristo sehemu nyingine duniani wanavyoteseka kwaajili ya huyu Yesu. 
Lee Strobel alikuwa mwandishi wa habari asiyeamini kwamba Mungu yupo, na nilipata kuangalia documentary yake lakini pia na movie yake mpaka alipokuja kumpata Yesu. Kutoka kutokuamini hadi kuamini, na kwavile muvi zinakuwaga nusu tu ya kile kilichopo kwenye kitabu, nataka kusoma kitabu chenyewe ili nijue kwa undani habari nzima na ukweli aliougundua ndani ya Kristo. Ili iniondolee maswali niliyonayo lakini pia maswali ambayo ninaweza kuulizwa na watu mbalimbali ambayo yeye alishayafanyia uchunguzi nikaweza kujibu pia kama nilipoelezea kuhusu umuuhimu wa kusoma Biblia hapa .
Hivyo ni vitabu vichache ninavyotarajia kuvisoma mwkaa huu, na nikimaliza nitakushirikisha vitabu vingine ambavyo ninatarajia kuvisoma katika mwaka huu. 
Kwa vitabu vingi vya Desiring God Organization ambavyo vingine nimeviweka hapa lakini vingine unaweza ukachagua mwenyewe kwenye website yao unaweza kwenda kwenye hii link. Lakini pia vingi unaweza ukagoogle mtandaoni na kuvipata.
Hivyo ni vitabu vichache ambavyo nitavisoma mwaka huu, lakini pia nikivimaliza nitakushirikisha vingine nitakavyovisoma katika mwaka huu.
Ubarikiwe,
Eunice?.

Related Posts

One Reply to “Vitabu Ninavyotaka Kusoma Katika Mwaka 2018”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *