Tips

Jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya safari za kimisheni (na vitu vya kubeba kwenye safari hizi).

Reading Time: 3 minutes

Mpaka sasa nimefanikiwa kwenda safari mbili????, najua kwasababu nimeandika hadi posti basi unategemea ningekuwa nimeenda nyingi?, hapana mbili tu. Lakini katika hizo napenda nikushirikishe namna ya kujiandaa. Safari yoyote ni maandalizi, zaidi ya yote huko unakoenda unaenda kufanya huduma kwahiyo maandalizi yake ni zaidi na vile ungekuwa unaenda kutembea.

Kabla haujaenda safari za kimisheni jiombee na iombee pia, unaweza ukaumwa kwasababu umebadilisha mazingira au vyakula, jiombee lakini pia omba Mungu akakutumie huko unakoenda. Unaenda kukutana na watu ambao Mungu anawapenda kama anavyokupenda wewe, omba Mungu akutumie huko unakoenda kwaajili ya utukufu wake.

Usiweke matarajio fulani, kwajinsi nilivyojifunza safari za kimisheni zinabadilika sana. Usitarajie jinsi ulivyopanga ratiba ndivyo itakavyokuwa, muache Mungu afanye kazi vile anavyotaka kupitia wewe,usitegemee chochote utakachokikuta ndio hichohicho kifurahie. Unaweza kulala tofauti na pale ulipozoea,ili mradi tu unaenda kumuina Yesu unapolala sio ishu kubwa sana.

Zikatae haki zako, kama unataka safari za kimisheni zikushinde basi fikiria haki zako unapokuwa huko. Jikatae, kubali kuwa mtumwa, kubali kuwaweka wengine mbele, zikatae haki zako zinazokutaka wewe kuwa bora kuliko wengine, wewe kulala, wewe kutumikiwa na kadhalika.

Kubali kutumiwa kama chombo na Mungu, kubali kukosa kula, kubali kusikiliza watu wenye shida hata kama umechoka, narudia tena zikatae haki zako.

Fuatilia kidogo kuhusu utamaduni wa watu unaowaendea, na ujiandae kuishi na kuukubali utamaduni wao. Usijifanye wewe mgeni sana au vyakula fulani hauli, au mavazi ambayo wao wanayavaa na mengine wanaoyapinga usivae hata kama kikawaida huwa unavaa, kuwa mmishenari ni kujitoa sana na kuwaonyesha watu unaoenda kuwahudumia upendo wa Kristo, namna Mungu anavyowapenda. Sasa ukifanya mambo ambayo yatawazuia wao kumkubali Kristo kwasababu yako, damu yao itakuwa mikononi mwako.

Jifunze sana Neno, soma sana neno. Jifunze pia kumsikiliza Mungu na ujue jinsi ya kumsikia ili hata unavyoenda umsikie anasemaje kwaajili ya watu wake. Msikilize Mungu na pia lijue Neno, hauendi kuelezea maisha yako bali upendo wa Mungu kwenye maisha ya watu wake hivyo mjue sana huyo unayeenda kumuelezea. 

Jiandae kifedha, uwe hata na hela kidogo ambayo itakuwezesha kufanya matumizi ya hapa na pale kama ni ya Tanzania au ubadilishe kama unaenda nchi nyingine.

Mara nyingi sishauri kuhusu simu kwasababu nilizoelezea hapa, kwahiyo kama hakuna umuhimu sana na umewaaga wote ambao ulipaswa kuwaaga na wanaelewa unaenda kihuduma nashauri simu usiitumie sana ili uweke attention yako yote kwenye huduma na sio kuwaza mambo yanayoendelea ulipotoka.

Vitu vya kubeba kwenye safari za kimisheni

 • Safari za kimisheni sio za matembezi kwahiyo haina haja ya kubeba nguo nyingi ili ukazionyeshe au kwa makusudi mbalimbali ambayo unaweza kuwa nayo, kama ni nguo basi beba zinaoweza kubadilishika au kuvalika kwa namna nyingi ila chache tu. Ambazo zinaweza kuchanganyika, koti na viatu ambavyo unaweza kuvirudia, mara nyingi sandals na raba.
 • Biblia
 • Daftari na peni- hii itakusaidia kuandika vitu unavyojifunza, itakusaidia kukumbuka majina au kuandika hata masomo kanisani.
 • Passport na kadi ya homa ya manjano- kama unaenda nje za nchi basi ni muhimu kubeba passport na kadi ya homa ya manjano.
 • Matumizi ya kawaida kama sabuni, dawa ya mswaki,deodorant, mswaki, nguo za ndani,chpa ya maji (kuna wakati unapoenda upatikanaji wa maji ni shida) nakadhalika.
 • kitabu– kitakusaidia wakati wa safari kwenda na kurudi usiboreke (kimoja tu kinatosha).
 • Fuatilia hali ya hewa ya unakokwenda kama unaweza ukabeba blanket, mwamvuli na masweta.
 • Kama unaweza ukajifunza lugha au maneno mawili matatu ya watu unaowaendea/ au ukabeba dictionary itakuwa ni jambo la muhimu sana.
 • Usibebe nguo za gharama au urembo wowote wa gharama,hautakuwa na muda wa kuuvaa.

Safari za kimisheni  ni nzuri sana na zinaweza kubadilisha maisha yako sana.

Ubarikiwe,
Eunice?

  Follow Eunice on Instagram 💜

  24, proud Tanzanian, taking life one day at a time and being less judgmental on this amazing journey. I haven't figured out everything in life, and i am okay with that.

  One Comment

  Leave a Reply

  %d bloggers like this: