Faith Talk

Safari za kimisheni na jinsi zinavyoweza kubadilisha maisha yako

Reading Time: 3 minutes

” Ni heri kuona kitu mara moja, kuliko kusimuliwa hicho kitu mara elfu moja”- Methali za bara la Asia.

 Umisheni ni jambo pana sana, ambalo linachukua maeneo mbalimbali. Kuna namna mbalimbali  ambavyo watu wanauelezea, kuna wale wanaofanya umisheni wa kila siku kwenye maisha yao, na wale wanaoenda au kupelekewa nchi za mbali. Ni swala ambalo lipo kwenye maswali kwenye vichwa vya wengi kwamba kama ni kweli kila mtu kaitwa kuwa mmishenari kama mtume Paulo alivyokuwa au wengine tuwafanye wengine kuwa wanafunzi hata hapa tulipo? Kufanya watu kuwa wanafunzi mahali popote ambapo tupo ni jambo zuri, lakini pia kwenda kwa watu wengine ni jambozuri.

Toka niko sekondari nilikuwa natamani kwenda safari za kimisheni kwani hostel niliyokuwa nakaa nilikaa na wanachuo ambao walikuwa wakienda safari hizo za kimisheni. Hivyo lengo langu la kwanza ni kuwa nikifika tu chuo niende safari hizi za kimisheni. Ila hali haikuwa hivyo kwani nilivyofika chuo niligundua wanaenda safari za kimisheni kwa muda wa miaka kadhaa na sio kila mWaka kama nilivyodhani. Lakini Mungu alinijibu maombi yangu kwani nilifanikiwa kwenda na organization nyingine nchini Uganda mwaka 2017 kwenye kambi ya wakimbizi ya watu wa South Sudan na maisha yangu yamebadilika toka hapo.

Safari za kimisheni zina umuhimu sana kwenye  maisha yako, kama yalivyobadilisha maisha yangu yanaweza kubadilisha na yako pia.

Kwa kupitia safari za kimisheni unaweza kujibu kiurahisi kama umeitwa kwenda kama mtume Paulo au umeitwa kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Kristo mahali pengine, kama haujawahi kwenda safari za kimisheni sio rahisi sana kujua kama umeitiwa umishenari labda Mungu awe ameongea na wewe kwa namna nyingine, ila kwenda safari za kimisheni ni njia rahisi ya kukufanya wewe ujue wito wako ulioitiwa.

Safari za kimisheni zinakufungua macho na kukufanya uone maisha ya watu wengine ambayo  ni tofauti na yako, lakini pia unaweza kuona kaka na dada zako katika Kristo jinsi wanavyoishi katika sehemu zao ambako wapo, mdogo wangu Angel alifanikiwa kwenda mkoa wa Rukwa kwa safari za kimisheni na alivyorudi alikuwa akinisimulia jinsi maisha yake na mtazamo wake katika maisha ulivyobadilika, na ni jinsi gani sisi wa sehemu nyingine tunaishi tofauti na watu aliokutana nao, hata jinsi makanisa yalivyo tofauti lakini wote tukimwabudu huyu Mungu mmoja.

Safari za kimisheni zinaweza kukufanya kuwa mtumiaji mzuri wa vitu ambavyo Bwana amekupa, nakumbuka baada ya kutoka Uganda, nakuona shida ya watu makambini niliwaza sana jinsi vile ninavyotumia hela zangu, muda, ujuzi na uhuru. Kwakuwa mara nyingi vitu hivi ninavyo, nilikuwa sijui ukivikosa maisha yanakuaje, baada ya kwenda Uganda niliona jinsi gani maisha yalivyo kwawasio navyo na hivyo naweza kusema sasa hivi nimekuwa mwangalifu na namna ninavyotumia vitu nilivyopewa.

Kukufanya kuwa mwanaombi, mara nyingi tunaacha kuomba na kusema hatuna vitu vya kuombea, safari za kimisheni zinakupa picha kubwa ya ukubwa wa vitu unavyoweza kuombea. Kuna muda huna hata haja ya kujiombea wewe, ila kuombea wale wanaoteseka kwenye nchi mbalimbali au mikoa mbalimbali, wale wanaotengwa au waliookoka wapya, ila utawaombeaje au utakumbukaje kwamba unapaswa kuwaombea kama haujawahi jua wao pia wapo?

Safari za kimisheni zinaweza kubadilisha maisha yako sana, nimeona namna gani zinabadilisha maisha yangu, zinaweza kukufundisha kujishusha, kuwa na moyo wa kitumishi, wa kuwaweka wengine mbele kabla yako, zinaweza kukufanya ukawajali ndugu zako katika Kristo kutoka sehemu mbalimbali lakini zaidi yako ukamwinua Mungu kwa mambo ambayo anayafanya sehemu mbalimbali kwaajili ya utukufu wake. Safari za kimisheni zinaweza kukufanya ukashuhudia makubwa ambayo Mungu anafanya, nimesikia shuhuda mbalimbali za jinsi watu walivyomuona Mungu kwenye safatri hizi, na wao kukua kiimani kwa kuwa wamemuona Mungu kwa namna ya tofauti akiwalinda na kuwaongoza. Nakushauri uende hata safari moja ya kimisheni kama ni mkoa mwingine au nchi nyingine, popote Mungu atakapo kupeleka, naamini  kwenye maisha yako hautabaki kama ulivyo.

Eunice?

Follow Eunice on Instagram 💜

24, proud Tanzanian, taking life one day at a time and being less judgmental on this amazing journey. I haven't figured out everything in life, and i am okay with that.

Leave a Reply

%d bloggers like this: