Lived Experiences (Opinions)

22-23 : Mambo 22 niliyojifunza kwenye maisha

Reading Time: 3 minutes

Tarehe 28/4, ni kumbukumbu ya miaka niliyozaliwa na jana nimekumbuka jinsi miaka 23 iliyopita nilivyokuja duniani. Ukiacha sikukuu, kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa ni siku ninayoipenda SANA. Ni siku ninayoipenda kwasababu inanikumbusha kwamba kuwepo kwangu duniani Mungu anamakusudi na mimi. Na kwavile ninakumbuka kuzaliwa kwangu na hivyo ninatimiza umri mpya na kwa mwaka huu nina timiza miaka 23, basi ningependa nikushirikishe mambo 22 niliyojifunza katika maisha yangu, bila kupoteza muda nikushirikishe.

 1.  Kila mtu hapa duniani anakusudi la kuwepo hapa, Mungu hajamuumba mtu yoyote kwa bahati mbaya, na Mungu hajatuumba ili tuishi peke yetu, bali na jamii kwahivyo huleta watu kwenye maisha yetu kwa kusudi na maana ya kutupa jamii ya kuishi nao.
 2. Upendo wa watu huweza ukaisha, na mara nyingi huwa na mipaka, lakini pendo la Mungu haliwezi kuisha.
 3. Maisha ni majumlisho ya machaguo mbalimbali ambayo tunafanya, labda tunajua au hatujui tunachagua jinsi maisha yetu yatakavyokuwa hapa duniani.
 4. Mungu anapenda tuwe huru pia, hata kwenye afya zetu za kihisia, mara nyingi tunafanya vitu ambavyo tunavijutia baadae kwasababu tu kihisia hatuko vizuri.
 5. Mara zote sikiliza na fuata sauti ya Roho Mtakatifu, hajawahi kosea au kumpoteza mtu.
 6. Sio watu wote ulionao kwenye maisha yako leo utakuwa nao kesho. Marafiki hubadilika na kubali endapo watabadilika.
 7. Kwenye kila jambo linalotokea una uamuzi wa kufurahi au kusikitika, kuwa na hasira au kuchukulia poa, kuwa na tumaini au kuwa na hofu.
 8. Mambo yaliyopo mbele ya maisha yetu ni mazuri sana, ni yale ambayo hatujawahi kuyaona wala kuyafikiria.
 9. Siku hazigandi, leo inaweza ikawa ngumu, au saa hili linaweza kuwa gumu ila litabadilika.
 10. Hakuna kitu/jambo/tatizo kinachodumu milele.
 11. Muda mwingine mlango wa kutokea anaotupa Mungu ni tofauti na vile tulivyowaza atafanya, lakini tujikumbushe tu Mungu huwa anatuwazia mema.
 12. Jifunze kuishi mazingira tofauti na yako, itapanua sana uwezo wako wa kufikiri na kujua mambo. Kwenye dunia watu wapo kwenye hali tofauti, ili kuweza kuelewa hali za wengine jifunze kuwaelewa na kuvaa viatu vyao muda mwingine. Kuwa na akili ni kujifunza kutoka makosa yako, ila kuwa na hekima ni kujifunza kutoka makosa ya wengine.
 13. Vitu huwa havibaki vilevile baada ya muda fulani, hata tabia za watu pia hubadilika.
 14. Ukimkasirikia mtu kwamba unamkomoa, mara zote huwa haumkomoi uliyemkasirikia ila unajikomoa wewe.
 15. Kuna watu wanaojitolea zaidi yako kwenye maisha kwahiyo usijedhani wewe umejitoa sana, au umefanya inatosha.
 16. Furahia maisha, mfurahie Mungu, fura
 17. Mungu ni Mungu wa neema na rehema, hata siku moja usijekumhukumu mtu kwamba ndio mwisho wake kiimani, huwezi jua Mungu atamrejesha katika muda gani.
 18. Usisikilize watu wanachokuambia uache kufanya, kama unajua kinampendeza Mungu na unamzigo wa kufanya,kifanye. unaweza ukawafundisha wao jinsi ya kukifanya au pia unaweza ukawa wewe ndo uliepaswa kukifanya hicho kitu kama kusudi lako. Kuonea aibu watu ni sababu kubwa ya vijana kurudi nyuma.
 19. Usimwombee mtu vibaya anapofanikiwa au kujisikia wivu, ishinde hiyo roho, maisha sio mashindano.
 20. Mahali ulipo, ndipo Mungu anataka uwepo. Usiangalie mwenzio yuko wapi, hata kama mnaishi nyumba moja inawezekana kabisa mkawa katika nyakati tofauti za maisha.
 21. Kuna siku utajisikia kama vile Mungu amekusahau au uko peke yako, kumbuka hata siku moja Mungu hawezi kukuacha, yuko karibu nawe zaidi ya vazi mwilini mwako, hata kuacha hata mwisho.
 22. Mara nyingine huwa tunachangia katika kutengeneza matatizo yetu sis wenyewe kwenye maisha, lakini hata katika hayo,Mungu ni mwaminifu sana kwenye maisha.
Katika siku ambayo nimetimiza miaka 23, hayo ndio mambo niliopenda kushirikiana nawe, ambayo nimejifunza katika miaka yangu iliyopita.
Ubarikiwe.
Eunice?

Click these social media icons to follow me on social media

Tanzanian, taking life one day at a time and being less judgmental on this amazing journey. I haven't figured out everything in life, and i am okay with that.

One Comment

Leave a Reply

Scroll Up
%d bloggers like this: