Tips

Mambo niliyojifunza kutoka kwa Meghan Markle

Reading Time: 3 minutes

Kama kuna watu walikuwa wanaisubiria harusi ya Prince Harry na Meghan Markle kwa hamu ni mimi.  Nimemfuatilia maisha ya Meghan kwa ukaribu sana, na nimependa vile anaishi maisha yake.
Kabla sijaongelea mambo ambayo nimejifunza kwa vile Meghan anaishi maisha yake,naomba niongee hili.

-Kama unatamani na wewe uolewe na prince ili uingie katika familia ya kifalme naomba nikukumbushe kuwa hauna haja ya kuolewa na prince kwasababu hiyo, wewe ni binti Mfalme tayari, tayari upo kwenye familia ya kifalme. Mungu wetu ni Mfalme anayedumu milele, ni Baba yako, kwahivyo wewe ni mtoto wa Mfalme, huna haja ya kutamani au kutaka kuolewa na mwana mfalme kwasababu yoyote, bali kusudi la Mungu nalitimizwe kwenye maisha yako.

Sasa natamani niongelee mambo niliyojifunza kuhusu maisha ya Meghan Markle, kwavile amekuwa kati ya wanawake wachache ambao mambo wanayofanya kwenye jamii yananiinspire.

Fanya mema kwaajili ya watu kila mahali unapokuwepo.
Kuna documentary nimeiangalia ambapo alikuwa anasaidia kupeleka vyakula kwa homeless people pale ambapo alipokuwa anaigiza, chakula kikibaki anawapelekea wale wenye njaa. Mara nyingi huwa tunadhani kufanya mema au kusaidia watu ni mpaka tuwe na hela au tuanzishe organization lakini kuwa na moyo wa kusaidia watu ni jambo ambalo unakuwa nalo moyoni, unalitengeneza, haina haja ya kufikiri mpaka utakapokuwa mtu fulani ndio usaidie, unaweza kusaidia hapohapo ulipo. Unaweza ukawatia moyo, na kuwasaidia wale watu ambao Mungu amewaweka kwenye maisha yako na karibu yako unaowaona. Ukitaka kusaidia watu anza na wale unaowaona.

Yale unayoyafanya yanakuandaa kule uendako
Ukifika kule Mungu amekupangia utagundua mengi uliyoyafanya yalikuandaa kwa kule Mungu anakupeleka, kama vile Daudi, Yusufu na mifano mbalimbali. Ukisoma bio ya Meghan Markle hasa kwenye website ya Royal Family utaona kuwa  yote aliyokuwa anayafanya kwenye maisha yake, yalimuandaa kwa zile kazi ambazo atazifanya kwenye familia ya kifalme.

Furahia maisha na uwe na mtazamo chanya kwenye maisha
Wakati bado natumia mitandao ya kijamii, nilikuwa namfuatilia Meghan Instagram, alikuwa anafurahia sana maisha yake, lakini pia alikuwa na mtazamo chanya kwenye maisha. Alikuwa single lakini hakuwa ameboreka, kuchukia au kuumia kwasababu yuko peke yake, ila alitumia huo muda kufurahia maisha yake na kusafiri.

SOMA:   Mitandao ya Kijamii

Unyenyekevu 
Katika yote niliyojifunza kwake hili nimelipenda, unyenyekevu na usiri. Nadhani kwa umaarufu na kwa mtu ambaye amekuwa naye kimahusiano mpaka sasa ndoa, ni vigumu sana kuwa mnyenyekevu na msiri. Lakini Meghan Markle ni mnyenyekevu hata kwa watu anaokutana nao lakini pia anaonekana ni mtu anayependa kujifunza na kusikiliza watu.

Kujitahidi kila siku kuwa bora na kujifunza
Meghan Markle amefanya kazi na watu wengi na leo nimesoma kuwa amejifunza Kispaniola na Kifaransa???, na hii pia inaweza ikatumika katika kazi yake mpya sasa kwenye ufalme. Kujifunza mambo mapya na kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa jana ni jambo zuri sana ambalo nimejifunza kutoka kwake.

Kuna vitu umezaliwa kuvifanya
Vile Meghan alivyotambuilishwa kama mchumba wa prince na alivyokuwa anaifanya hiyo kazi ya kiuana mfalme, unaona kabisa kwamba ile kazi amezaliwa kuifanya. Maana alikuwa anaifanya kwa moyo, kwa nguvu na kwa furaha. Vile vitu umepangiwa kuvifanya utavifanya kwa moyo na kwa furaha.

Mungu akiwa amekupangia kitu haijalishi nani amekutangulia
Kama nilivyosema naamini hiyo kazi Mungu alimpangia yeye kufanya, na ndio maana amekuwa yeye katika kipindi hiki.

Jipende na jikubali vile upo- watu pia watakukubali
Nakumbuka wakati wanaanza mahusiano Meghan alisemwa sana kuhusu yeye kuwa mtu mweusi lakini kwenye interview yao ya kwanza ya uchumba alisema anajikubali na anajivunia vile alivyo. Mungu amekuumba vile ulivyo katika kila mahali, jikubali vile ulivyo. Jikubali kabisa.

Usimdharau mtu, wapende watu na ishi na watu wa aina yote
Katika maisha yake na jinsi alivyokuwa akiishi alijichanganya na watu tunaodhania wanaheshima na watuj ambao sisi tunadhani hawana hadhi. Hakudharau watu wote na hili ni jambo ambalo nimejifunza sana kutoka kwake.

SOMA :   Kwa wasio na baba

Mungu atamleta mtu wa kufanana nawe
Katika yote aliyoyafanya na ukiangalia anayoyafanya Prince Harry yanafanana, hapo nikaamini kweli Mungu atakuletea wa kufanana na wewe.

Mungu anampango na maisha yako ambao utamshangaza kila mtu
Hakuna mtu aliyefikiria kwamba atakuja kuingia kwenye familia ya kifalme, na vile kidunia ni ishu kubwa sana kwa hayo atakayoyafanya baada ya kuingia katika familia ya kifalme,hata waliokuwa wanaigiza nao hawakuwahi kufikiri kwamba mtu wanaeiigiza naye atachukua kazi kubwa kama hiyo ya kifalme. Kama Yusufu, kama Daudi, kama Esther, Mungu anampango mkubwa na maisha yako ambao utamshangaza kila mtu.

Na hayo ni mambo machache niliyojifunza kwenye maisha ya Meghan Markle, na ambayo  nimeyapenda.

Eunice??.

Follow Eunice on Instagram 💜

24, proud Tanzanian, taking life one day at a time and being less judgmental on this amazing journey. I haven't figured out everything in life, and i am okay with that.

One Comment

Leave a Reply

%d bloggers like this: