Eunice Tossy/ April 15, 2019

Last Updated on

eliud

Nilikutana Eliud mkoani Mbeya, wakati nasoma. Na Eliud, kijana mwenye umri wa miaka 29 alikuwa anaimba hadi kwenye maconcert yaliyokuwa yakiandaliwa MUST, na pia kwenye mikesha yetu ya mwaka mpya. Kuona kwamba yupo kwenye muziki hadi sasa mpaka anashindanishwa kwenye tunzo za uimbaji huko nchini Kenya na kushirikiana na wasanii wanaomwimbia Kristo, ni kitu kikubwa sana, kwake nimejifunza dedication, kuwa humble na kuheshimu kile ulichoitiwa. Nimepata heshima ya kumuuliza Eliud maswali mawili matatu, let me assure you kwamba he will inspire your life kwakweli.

Tupate mawili matatu kutoka kwa Eliud Martine.

eliud

 

Tuambie kidogo kuhusu safari yako ya mziki?

EM : Nilianza uimbaji nikiwa darasa la tano ambapo nilikuwa nikiimba kwaya na kufundisha kama mwalimu wa kwaya. Nimelelewa katika familia ya kikristo ambapo nilijikuta nashawishika kuimba na kikaanza kuimba nyimbo zangu baada ya kwenda chuo, na rasmi mwaka 2016 nikaachia wimbo wangu uitwao “TULIA KWA YESU” na ndipo safari yangu ya uimbaji ilipoanza. Hadi sasa nna nyimbo sita YouTube ambazo ni videos &audio.

Unajiepushaje na majaribu kama kijana?

EM : Majaribu hayana budi kuja lakini Mungu hutupa njia ya kutokea na kuniimarisha.

Kujulikana kumebadilishaje maisha yako? (kwa ubaya na uzuri)

EM : Kujulikana kumenisaidia kutengeneza connection mbalimbali na kunikutanisha na baadhi ya waimbaji wenzangu.

What’s your advice for the aspiring musicians?

EM : Ushauri kwa waimbaji wenzangu na wanaochipukia ni kuwa, wasikate tamaa maana Mungu kaweka utofauti kwa kila mtu katika huduma na vipawa ni tofauti, kukata tamaa siyo njia ya ki Mungu.

MMMMM

Una malengo gani na muziki unaofanya?

EM : Nina malengo makubwa, kwanza kuitangaza injili sehemu mbalimbali na kutangaza Neno la Mungu kwa watu mbalimbali na pia kuwafanya wawe watoto wa Mungu.

Muziki umekusaidiaje kukua kiroho?

EM : Mziki umeongeza imani na kuimarisha mahusiano yangu na Mungu maana kila nikitaka kuandika nyimbo ni lazima nikae chini nimuombe Mungu anipe ujumbe na message nzuri itakayogusa maisha ya mtu.

What’s your advice for your fellow young men?

EM : My advice for young men ni kwamba wasiogope kumwimbia Mungu na kukimbilia kuimba muziki mwingine kwani pia hata huku unaweza kuimba muziki mzuri ukalitangaza jina la Yesu na kuwafanya vijana wengine kuijua kweli.

Ni mambo gani umejifunza katika safari yako ya mziki na maisha kwa ujumla?

EM : Nimejifunza kutokukata tamaa na kusubiri siku yako au kesho yako ambayo ni kesho ya mafanikio.

 

Unaweza kumfollow Eliud Instagram :  Eliud Martine

Na kuangalia nyimbo zake Youtube:  Eliud Martine

 

ABG.

 

Share this Post

About Eunice Tossy

24, proud Tanzanian, bookworm, beach lover, loud laugher,conversationalist, deep thinker, public foodie, authentic writer and globetrotter.

1 Comment

  1. Asante sana tossy kwa hatua hii MUNGU akubariki sana na akupandishe juu zaidi

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*