Your Guide To University Life

Goal setting : Jinsi ya kujiandaa kufikia malengo yako chuoni (kwa first year)

Reading Time: 2 minutes

(Kwa kusoma posti mbalimbali zinazohusu maisha ya chuo, bonyeza hapa.)


Hello it’s me again!

Sababu pekee naandika makala kuhusu maisha ya chuo, ni kwasababu natamani wengine wafanikiwe katika maeneo ambayo naona nilifanikiwa, lakini pia wasishindwe katika maeneo ambayo Mimi nilishindwa.

Kitu kimojawapo ambacho natamani kuwa ningekifanya kabla sijaenda chuoni ni kuweka malengo. Malengo ambayo ningetaka niyatimize katika miaka yangu ya chuo, miaka minne ambayo nilikuwa chuo.

Nadhani hatuweki malengo ili tubanwe Ila ili tuwe na nidhamu.

Malengo yanasaidia kukupa self control na kukupa kitu unacho aim, na hivyo badala ya kuishi tu bila direction na kupoteza muda unakuwa na kitu kinachokuongoza namna unavyoishi.

So kwavile Mimi sikuwa na wazo hili toka hapo, nataka kushare na wewe aina za goals ambazo naona kama mwanachuo unayeenda kwa Mara ya kwanza zitakusaidia sana. Panga goals zako kabla haujaenda, ili uende ukiwa tayari na mpango wa kuzitimiza.

Goals zenyewe ni;

Academic goals

Hapa weka malengo kuhusu masomo yako, unatamani ufaulu wako uweje, utasomaje, matumizi ya resources za chuo and etc. Unapoenda chuo kwa miaka yako unayoenda, unatamani kufikia wapi academically? Na sio lazima liwe jambo la kutisha, weka realistic goals ambayo unaweza kuzifikia.

Hapa niongezee na professional goals…. Unataka kujifnza chochote kipya ukiwa chuo? Na je akati upo chuo utajiendelezaje professionally au kujiendeleza kwa kile unachokisoma nk.

Financial goals

Hapa kwenye pesa utakazopata, boom lako unapanga kulitumiaje? Je, matumizi yako yakipesa yatakuwaje? Je, unatamani kuanzisha biashara? Unatamani hela uliyonayo ikuingizie zaidi? Nk

Jiweke malengo vile unataka financial situation yako iwe.

Ideas za biashara unazoweza kuzifanya ukiwa chuo – (https://youtu.be/jgE9MA8mSak)

Personal goals

Binafsi unatamani uweje? Ukue katika eneo gani as a person? Ujifunze kitu gani kipya ukiwa chuo? Unataka ufanye sports, ufanye mazoezi, ule balanced diet or how will your personal life be like?

Hapa niongezee na relationship goals, unaweza kuongezea vile unatamani kurelate na watu au hata kuyaendesha maisha yako kwenye mambo ya kijamii(social life).


Na hayo mdo malengo ambayo natamani uyaweke kabla haujaenda chuo, ili uyafanyie kazi ukifika chuo.

Eunice💜

Follow Eunice on Instagram 💜

24, proud Tanzanian, taking life one day at a time and being less judgmental on this amazing journey. I haven't figured out everything in life, and i am okay with that.

2 Comments

Leave a Reply

%d bloggers like this: