Lived Experiences (Opinions)

Maisha ni magumu, maisha ni mazuri

Reading Time: 2 minutes

Natamani niandike kuhusu hili ili moyo wangu utulie.. Lakini pia ili ni process what I am feeling.

Najua kila mwaka tunakuwa tunandoto za kuona kuwa labda huu ndio mwaka mwepesi kuliko uliopita. Nilisema mwaka Jana kwamba mwaka Jana ulikuwa mgumu, nashangaa pia nasema hivyohivyo kuhusu mwaka huu. Ni kama jinsi ninavyoendelea kukua ndio changamoto zinaongezeka au magumu yaliyo makubwa ndio yanakuja.

Kama mwaka huu, nimepitia mengi mpaka ikafika kipindi moyo wangu ukaacha kufeel chochote, unajua ile moyo umeumizwa mpaka umejenga ukuta kwa yatakayo kuja yasikuumize..

Ubaya ni kuwa yanaacha kukuumiza, maana inaonyesha kiasi gani umechoka.

Hapo ndipo ninapoelekea…

Kwasasa bado naumia, bado nachoka. Maana kila linalokuja nalibeba, na kuumia, ukitegemea habari njema inakuja nyingine inayokuumiza zaidi na unaendelea kuchoka kama ile habari ya kwanza ilivyokuacha.

Just tired. Tired of everything.

Mwaka huu nahisi nimelia sana, nimekaa chumbani kujifungia mbali na dunia, nimelia sana.

I have cried myself to sleep, in many nights..

Just tired

Ukweli ni kuwa sijachoka kwasababu ya mambo yangu, nahisi Niko vizuri kuyaweka ya kwangu pembeni na kuumia kwaajili ya wengine.

Nahisi Nina maswali ya kwanini jambo fulani linatokea kwenye maisha ya wengine..

Jana nimesikia kuna jirani yangu amefariki, amefariki akiwa mdogo sana. Mdogo wake ameanza mitihani ya taifa leo… My heart broke for him.

Nikajiweka kwenye viatu yake, nikaumia kwasababu yake, nikaendelea kuchoka.

Maisha yanachosha, yana ugumu ambayo unajiuliza umekujaje..

Ukweli ni kuwa sijaenda kanisani kwa 100% toka mwaka uanze, kama nimeenda basi nilienda sababu nipo home na mama alinilazimisha.

I still believe there is God but sometimes it gets hard.

It is hard to find the connection that I had.

Kuna muda nawaza kama jina la blogu yangu ni sahihi kwaajili yangu, kwasababu mwaka huu nimepata shida sana ya kusoma Biblia.. Je niendelee kujiita abiblegirl?

Kuna muda sina majibu ya maswali yote niliyonayo,

Kuna muda natamani nirudi kuwa mtoto kama nilivyokuwa bila kitu cha kukiwazia,

Kuna muda nashindwa kuelewa kwanini vitu fulani hutokea,

Kwanini kuna watu wanapigania maisha yao sasa hivi hospitali, na kuna wengine wanaachana baada ya kupendana sana kwa muda?

Kwanini maisha huwa hayaendi kama tunavyopanga?

Kwanini kuna muda tunaomba kwa kuumia na mambo hayatokei?

Kwanini maisha yanatuumiza?

Kwanini mabaya yanatokea?

Nahisi kama maisha yalikuwa mepesi na mazuri nilipokuwa mtoto..

Sasa hivi naona maisha ni magumu, na kwa vile bado tunacheka, na kunasiku tunafuraha naona maisha ni mazuri.

Bado siyaelewi maisha.. Lakini labda sio kazi yangu kuyaelewa, kazi yangu ni kuyaishi hivyohivyo yanavyokuja.

Eunice💜

Follow Eunice on Instagram 💜

24, proud Tanzanian, taking life one day at a time and being less judgmental on this amazing journey. I haven't figured out everything in life, and i am okay with that.

Leave a Reply

%d bloggers like this: