Umuhimu wa kuiombea nchi yako kwa mzigo mzito

Reading Time: 5 minutes Heri ya sikukuu ya Muungano, Tanzania. Woow, Muungano, miaka 55 sasa. Bado nafikiria hekima za viongozi wetu kukaa chini na kuona umoja ni muhimu kuliko utengano, mambo yamebadilika siku hizi vijana wengi hatufikirii hivyo, tunashindana sana kuliko kushirikiana but hiyo ni blogpost ya siku nyingine. Leo ni kumbukumbu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Tanzania (am yet to go to Zanzibar, na nikienda rest assured i will share a post about it). Kama unanifahamu vizuri unajua naipenda Tanzania toka moyoni, like #Tanzaniapleaseadoptme kind of love. Lakini haikuwaga hivyo miaka yote, nakumbuka nilipokuwa secondari, Jangwani, ndipo huo upendo ulipokuja.